Saturday, October 22, 2011
Kasheba
Kila wakati nasema nitajitahidi kuwa hewani zaidi lakini lazima nikubali kwamba ratiba yangu ya shule na kazi ni nzito na ndio maana inashindikana. Usiku huu nikiwa kwenye blog ya michuzi nikaona post moja juu ya Ndala Kasheba ikanikumbusha mbali sana na nikaona ni heri kutafuta muda wa kutoa comment.
Nakumbukua siku moja maeneo ya Kawe Club kulikuwa na na bendi ya muziki ikifanya mazoezi. Kwa mapenzi yangu makubwa ya muziki nikaanza kuuliza ilikuwa bandi gani? nikaambiwa ilikuwa ni mchanganyiko wa mastaa wa muziki wa bendi Tanzania. Namkumbuka mwanamziki mmoja aliyeyenivutia sana wakati ule, alikuwa akipiga gitaa kwa umahiri mkubwa na kuimba na siku moja nikamfuata na kumsalimia ijapokuwa kwa hali ya woga na kumwambia kwa jinsi gani ninavyopendelea muziki wake. Alikuwa amevaa shati la kitenge na kofia ya mkeka akaniambia jina lake ni Ndala Kasheba. Nilikiuwa nimemsikia mara nyingi kwenye redio na nafasi ya kuongea nae ilikuwa kama ni ndoto, sijawahi kusahau hata siku moja makutano yangu ya mara ya kwanza nae kwani tulionana mara nyingi baada ya hapo kila jumapili aliyokuja pale Kawe Club.Na nakumbuka kwa huzuzni kubwa siku niliposikia kwamba amefariki dunia. Nilikuwa katika mikakati ya kutaka kumuona akija kwenye ziara ya New York lakini haikutokea. Leo natoa heshima kwa mmoja wa wanamuziki mahiri kabisa duniani Fred Ndala Kasheba. Utabakia kuwa mmoja wa wawakilishi bora zaidi kwenye fani ya muziki wa Kiafrika.
Subscribe to:
Posts (Atom)