Sunday, January 11, 2009

Taifa Stars

Kwa muda mrefu sasa najaribu kuifuatilia timu yetu ya taifa kwa karibu.Na kama na wewe ni mfuatiliaji mzuri hutapingana nami ninaposema timu hii hairidhishi.Ni kweli tumepiga hatua kutoka tulipokuwa miaka mitatu nyuma,lakini matokeo yasiyotabirika kama kushindwa tunapocheza na timu dhaifu kama Somalia au Cape Verde katika michezo ambayo inahesabika kama ya kuchukua pointi kunakuwa kunaacha maswali mengi ya nini kitatokea tutakapofika Ivory Coast.
Sio lengo langu kumvunja mtu yeyote moyo,na kweli mpira ni dakika tisini, lakini ni vizuri kujiuliza maswali wakati mwingine na sio tu kutegemea miujiza.Timu zinazofanya vizuri hazifanyi hivyo kibahatibahati tu ila ni maandalizi na mbinu nzuri za kimchezo.Wachezaji wazuri wenye kujituma na kujiamini wawapo uwanjani ni chachandu kamili ya ushindi.Kila la heri Taifa Stars kwenye kutafuta mshindi wa tatu kombe la Challenge,Tupe raha watanzania.

No comments:

Post a Comment