Friday, December 17, 2010

Kiberenge, Dedication

Ningependa kuwaomba radhi marafiki zangu kwenye facebook kwa kuwa tag kwenye nyimbo zangu. Wakati nilipoamua kuingia facebook ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya familia na marafiki, nimejitahidi niwezavyo kuiacha facebook iwe hivyo lakini every now and then nakubali urafiki wa watu tusiofahamiana. Ninajitahidi kukataa urafiki wa watu nisio wafahamu lakini hawa ni watu wanaosikiliza nyimbo zangu na inaniuma kukataa kuwa marafiki nao ukuzingatia nusu ya watu ninaowaita marafiki hata hawajui kwamba mimi ni msanii.

Nimejitahidi mara nyingi kuwatumia nyimbo zangu watu wa karibu na mimi lakini wengi wao hata hawahangaiki kufungua e mail zenye nyimbo zangu na ndio sabau kubwa hawajui kazi zangu. Ila napenda niwashukuru marafiki wangu wapya waliopo east Europe na Asia ndio mnaonifanya niendeleze libeneke hili leo hii. Mimi sitengenezi mziki kwa ajili ya biashara kama wasanii wengine bali kwa ajili ya kueneza uamko kwenye jamii. Si kwamba sina shida ya hela bali sina shida hela kama asilimia kubwa ya wasanii wa kitanzania.Sijaridhika na maisha bado nachakarika kuyaboresha lakini haina maana kama nitaboresha maisha yangu na kuwaacha watu wengine wakiteseka bila kujua sababu za msingi. Maisha yangu kisanii ni kusambaza ujumbe kwa watanzania ya kwamba hawaitaji kuridhika na walichonacho but life can get better if you know what is the problem and how to fix it.

Macho yangu yalikuwa yamegubikwa na pazia la kutokuelewa kama watanzania wengi ambao hawajakulia kwenye wimbi la umasikini ila kwa bahati nzuri I learned how the other side lives in an earl age. Nawashukuru ma class mate wangu kwa kunionyesha reality of life maana leo hii ndio mnao nifanya niangalie maisha kutokea kwa chini. Maisha ni mapambano na sitegemei kuishiwa nguvu wakati wowote wa karibuni. Ningependa kuona Watanzania wenzangu wakiukumbatia uelewa siku za karibuni na kuanza kui –chalenge Taboo. Ninaelewa lugha ninayotumia sio sahihi kwa kila mtu kwenye jamii lakini kama msanii lugha chafu ni kama zana niliyokabidhiwa kuleta uamsho kwa wasililizaji. Tatizo pekee nililonalo ni kwamba mtandao ndio tegemezi langu kubwa la kuwafikia watu na ndio maana sifurahii watu waishio nje ya Tanzania wanaoendelea kukubali ujinga wakati wananafasi kubwa ya kupata picha sahihi. Kwahiyo wakati ninaweletea nyimbo zangu kama kiberenge muelewe mapambano yanaendelea.

Ninaamini maendeleo yanawezekana kwenye nchi yetu. Ninaamini wananchi wa Tanzania wanataka maendeleo. Ninaamini kama wananchi wangepewa mbinu za kueleweka za kupambana na umasikini na maradhi Tanzania ingekuewa ni nchi bora,Tatizo ni kwamba baadhi ya viongozi tulionao are not even fit to run a village post office.

No comments:

Post a Comment