Monday, March 21, 2011

Tanzania inajifunza nini kutoka nchi za kiarabu?

Nimekaa kimya mda mrefu kwa ajili ya kubanwa na shughuli zangu binafsi lakini si kwamba nilikuwa sioni kinachoendelea kwenye nchi za Afrika Kaskazini. Tumeona mapinduzi kwenye za Tunisia na Misri. Machafuko yanayoendelea leo kule Libya. Na swali linalonijia kichwani je tunajifunza nini? Serikali ya CCM inajiandaa vipi kulinda madaraka yake?
Tumeona CHADEMA wakiandamana kila leo na serikali ikijaribu kwa kila njia kupigana nao je ndio kusema ukiona mwenzako ananyolewa basi na wewe tia maji ? Tunasikia watu kama wakina Sophia Simba wakisema eti ni mataifa ya nje yanayowashawishi CHADEMA kuandamana kwa faida ya nchi gani? naweza nikaandika haya maswali mpaka kesho wakati ukeli ni kwamba nahitaji majibu.

No comments:

Post a Comment