Habari za masiku wajameni? Nilikuwa nimebanwa sana na kupiga kitabu muda wa kupost huku ukawa haupatikani. Nasikitika ya kwamba kwa kipindi chote nilichokuwa kimya kuna mambo mengi yaliyokuwa yanatokea ulimwenguni lakini sikupata nafasi ya kujadiliana na watu wangu. Sasa mwaka unakaribia kukatika na ni muda wa kuanza kutafakari yale yote yaliyotokea mwaka huu na kuweka maazimio ya mwaka mpya.
Mwaka wa 2011 ulikuwa ni mwaka wa faraja sana kwangu, pamoja na kubanwa sana na masomo baraka za mwnyezi Mungu nimeziona. Tukiachana na mambo binafsi, naamini mwaka huu pia ulikuwa na mafanikio sana kwa Dunia hususani ulimwengu wa waarabu wa Afrika. Najua wengi wa marafiki zangu walinipinga sana kwa sababu za kutompenda Ghadafi lakini nadhani ni kutokana na uelewa wao mdogo kuhusu yule shatani pamoja na propaganda za Tanzania za kuamini kukataa uongozi mbaya ni kukataa Uafrika. Wakati tunaelekea mwisho wa mwaka na mimi kuanzia kesho nitaweka topten ya matukio yaliyokaa nami zaidi mwaka huu .
No comments:
Post a Comment