Thursday, March 12, 2009

Taifa Stars 2

Niliangalia dakika za mwisho za mpira kombe la CHAN kati ya Stars na Zambia kwa masikitiko makubwa.Ushindi ulikuwa karibu kiasi cha kuweza kuulamba na kusikia utamu wake lakini bahati haikuwa yetu.Sio siri mpira wa Tanzania umepanda kiwango sina wa kumlaumu kwa kushindwa kupata ushindi maana asiyekubali kushindwa sio mshindani.Hongera sana timu ya Taifa tukiongeza bidii labda na sisi siku moja tutawatetemesha wengi kwenye ulimwengu wa soka.

No comments:

Post a Comment