Kwa muda mrefu nimekuwa nikiota kuona mchezaji wa tanzania akicheza ulaya.Kwa sisi tuishio nje ya Tanzania tunatamani kusema mchezaji huyu ni wa Tanzania lakini bado haijawahi kutokea tunabaki kusema huyu ni Mwafrika mwenzetu.Kama Mrisho Ngasa atafanikiwa katika majaribio yake ya West Ham basi atakuwa ni mchezaji wa kwanza wa kitanzania kwenye ligi kubwa ya ulaya.
Nakutakia mafanikio mema kwenye majaribio yako,na hata kama yasipoenda sawa sio mwisho wa njia.Itakuwa furaha next time nacheza gemu kwenye PS3 au Xbox na kuona jina la Mtanzania ndani.
Kila la Kheri.
No comments:
Post a Comment