Mara ya mwisho kuandika kuhusu uchaguzi ilikuwa kabla Sugu hajachukua fomu za ubunge lakini alikuwa ameshatangaza nia yake ya kuua[ Ruge upo hapo] Slaa alikuwa hajajua kama ndio atakuwa mgombea wa uraisi wa Chadema lakini alikuwa ameshaoa mke wa mtu na kama kawa CCM walikuwa wanaendelea kufanya serkali na chama kuwa ni kitu kimoja.
Mimi sio mwandishi wa magazeti kwa hiyo ninaelemea upande mmoja na wala hilo sikatai. Mimi ninaweza kusema kuwa na bahati ya kuwa mmoja wa watu wenye upeo tofauti kuhusu hali nzima ya siasa na maisha ya mtanzania na nina bahati pia ya kuwa na marafiki walio kwenye level hiyo hiyo kwa hiyo sihitaji sana kulazimisha point kwa sababu wasomaji wangu wananielewa. CCM imekuwa madarakani kwa muda mrefu sana kushindwa kuleta maendeleo. Kwa katiba ya Tanzania tunategemea chama tawala kifanye mabadiliko ya kimaendeleo kwa miaka mitano kikishindwa mwingine apewe nafasi. CCM imeshindwa sasa kwa nini hatuwapi wengine nafasi?
Niliandika kwenye post ya kwanza sababu zinazofanya CCM inakuwa gumu kutoka madarakani. Kwa wale ambao hamkupata kusoma hiyo post basi kwa kifupi pamoja na mambo mengine mengi ni kwamba baada ya mfumo wa chama kimoja kufa CCM iliendelea kushikilia vitega uchumi vyote walivyokuwa navyo ambavyo vinatakiwa kuwa mali ya wananchi. Chama na serikali vilikuwa ni kitu kimoja,wananchi walijenga viwanja,kumbi za mikutano na kadhalika kwa sababu walikuwa hawana hiari. Kwa msingi huo baada mfumo huo kufa serikali ilitakiwa irithi hivi vitega uchumi badala yake wakakiachia chama. Hii imesababisha mizani kuelemea upande mmoja kwa sababu vyama vingine vyote vimeanzia kwenye sifuri huku CCM wakianzia kwenye tisini na tisa.
Leo hii nata niwapongeze CHADEMA kwa sababu wameonyesha nia yao ya dhati ya kumthamini mtanzania na sio tu tamaa ya madaraka. Kwenye chaguzi zilizopita ilikuwa ni kawaida kwa mwenyekiti wa chama kuwa ndio mgombea wa uraisi lakini CHADEMA wamelibadilisha hilo kwa kumweka mtu anayekubalika na wanachi wengi wenye akili timamu. Vile vile vijana wengi wamejitokeza zaidi kwenye medani ya siasa [kila la heri Mr 11] hii inaonyesha imani iliyopo kwenye chama hiki. CCM ina vijana wao[ the next generation ya mafisadi] wanaonadiwa kwa nguvu sana na this generation, kwa hiyo mchuano utakuwa ni mkali.
Kwa kumalizia napenda niwakumbushe wote umuhimu wa kupiga kura. Siku ya uchaguzi mkuu usikubali mwenzio akuamulie nani akutawale bali amua wewe mwenyewe. kura moja inaweza badilisha nchi.
Aley,
ReplyDeleteNakubaliana na wewe mazima mkuu. Giyo kitu imekuwa ikiniumuza sana kwa wakati wote huu baa ya kuingia kwenye vyama vingi. Cha kushangaza sijaona wapinzani wamechukua hatua gani kukabiliana na swala la SISIEM kuodhi mali zilizo jengwa na kuendelezwa kwa nguvu na kodi za watanzania, naamini wanaweza kukilazimisha chama hata kwa kupitia mahakama kurudisha mali hizo kwenye serikali kuu. It totally unfair to compete with TADEA which might not have even a single motor vehicle against a party which claim to own almost all big stadium in the Country with offices all over the country... Its time for change guys lets do it...
Chama chochote kitakachoingia madarakani kinabidi kirekebishe hii ishu. Ni mbaya sana mwanangu
ReplyDelete