Wednesday, June 9, 2010
Taifa stars kipute na Brazil maendeleo yanaonekana
Malalamiko mengi yalitolewa kuhusu kocha aliyemaliza muda wake bwana Maximo. Kuanzia kwenye uchaguzi wa timu hadi kwenye perfomance ya timu,lakini ukichunguza sana utaona ya kwamba watu hawakumfurahia kwa sababu kocha aliapewa uhuru wa kuchagua timu yake mwenyewe, na swala laperfomance lazima tukubaliane kocha alikuwa anafanya mafunzo yaliyotakiwa kutolewa kwenye vilabu watokapo wachezaji badala ya kufanya kazi yake kama kocha wa timu ya taifa.
Kwa muda mrefu tulishazoea kuwalazimisha makocha katika uchaguzi wao wa wachezaji hata kama wachezaji hao hawaendani na staili ya kocha. Kwenye mechi zidi ya Brazili kulikuwa na malalamiko kama hayo wakati ukweli ni kwamba hata Dunga amefagilia uchezaji wa timu yetu.Timu ilionyesha nidhamu, na kijiamini,na ninaamini kufungwa kwetu nikutokana na kukosa udhoefu kama waliokuwa nao wapinzani wetu.
Kama kuna kitu kukubwa kilichomuumiza akili Maximo katika uchaguzi wa timu ni maumbo ya mwili. Wachezaji wengi dunia hii ya leo wanamaumbo makubwa kitu ambacho ni adimu bongo. Watanzania kwa wastani tuna maumbo madogo tofauti na nchi nyingi. Ili tuweze kufanikiwa tunahitaji tujue jinsi yakutumia walakini wetu kama faida, tuweze kuleta ladha tofauti dimbani kama Ngasa.
Sababu kubwa inayoleta matatizo kwa kocha yoyote wa kigeni bongo ni ukosefu wa mafunzo ambayo ni basic kwa wachezaji wengi.Kocha wa timu ya taifa kazi yake ni kupanga mikakati ya ushindi na si kufundisha basics kama stamina na ball control. Tatizo la timu zetu nyingi bado zinatoa mazoezi ya mwaka arubaini na saba na hazina hata mazoezi ya vitu vizito kuongeza stamina kwa wachezaji. Lazima tuelewe kwamba nchi za wenzetu kwenye ngazi ya kilabu wachezaji wanapewa restrictions kwenye chakula na pombe. Wakati hali hii haipo kwenye asilimia kubwa za timu zetu ni juu ya mwanamichezo mwenyewe kuamua nini chakula au kunywa.
Ni kweli magoli tulipigwa lakini nani ambaye hakutegemea hilo?Cha muhimu ilikuwa nikujitangaza na hilo limefanikiwa. Kila la heri kwa kocha mpya you have some big shoes to fill.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment