Saturday, June 5, 2010

Tanzania kulipa Brazil ulakini upo wapi?

  mijadala imeibuka sehemu nyingi juu ya malipo ya mamilioni ya fedha yaliyotolewa ili kuileta timu ya taifa ya brazili kupambana na tanzania.Kwa watu wengi haina sense pale nchi masikini kama hii ambayo hata bajeti ya taifa inachangiwa na wahisani inapoamua kutupa hela.Ki kawaida ningekuwa mtu wa kwanza kupingana na swala hili lakini sitaki kikurupika tu lazima niangalie pande zote za sumni.Ni kweli kabisa hii hela ingeweza kufanya mambo mengi mengine ya maana lakini leo hili ndio jambo la maana.Kama kweli tunataka kuitangaza nchi yetu duniani basi lazima tulopod gharama zake,toka lini ukapeleka matangazo yako kwenye vyombo vya habari yakatangazwa bure? Lazima tukumbuke waamichezo wetu wengi wamekuja na kuondoka bila kupata nafasi ya kuonekana kimataifa. Hii ni nafasi kubwa kwa wachezaji wetu kuonekana ulimwenguni,ni nafasi kwa watu kufahamu kuna nchi inayoitwa Tanzania na ipo Africa na sio Carribean. Kila la heri Taifa stars,wachezaji wetu this is your time to shine. Mungu ibariki Tanzania

No comments:

Post a Comment