Aliyekua kiungo wa Simba na timu ya taifa ya soka, Taifa Stars, Haruna Moshi 'Boban', amepoteza nafasi ya kuwa mtanzania wa kwanza kushiriki katika michuano ya Ligi ya Europa baada ya kuvunja mkataba wake wa kuichezea klabu ya Gefle IF ya Sweden aliyoanza kuichezea Novemba mwaka jana.
Klabu ya Gefle IF, itaanza kucheza mechi yake ya kwanza ya hatua ya makundi ya Ligi ya Europa dhidi ya Liverpool.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakala wa mchezaji huyo, Damas Ndumbaro, alisema kuwa licha ya Boban kupoteza nafasi hiyo, amesikitishwa na maamuzi ya kiungo huyo kuvunja mkataba na timu hiyo kwa sababu alizozitaja (Boban), ambazo zinaonekana wazi kwamba si za msingi.
Ndumbaro alisema kuwa wakati akiwa Gefle, Boban alikuwa akilipwa mshahara wa kila mwezi wa Dola za Kimarekani 5,000 (sawa na Sh. Milioni 7.4), na kushangazwa na kauli kuwa kiungo huyo alikuwa hataki fedha hiyo ikatwe kodi.
Ndumbaro alisema vile vile kuwa, Boban alikuwa akihitaji kulipwa fedha zinazotokana na mapato ya milangoni, pengine kama utaratibu wa nchini ulivyo , jambo ambalo katika nchi zilizoendelea halipo.
Alisema kuwa kabla ya kueleza hoja hizo, Boban alianza kukacha mazoezi ya timu kwa kudanganya kuwa ni mgonjwa, jambo ambalo lilimfanya akose motisha ya Dola za Kimarekani 200 kwa kila mechi (sawa na Sh. 295,000), ambazo zilikuwa zikitolewa na uongozi wa klabu hiyo.
"Pamoja na yote hayo, bado kampuni yangu itaendelea kumtafutia timu nyingine, ila ni lazima klabu itakayomhitaji kulipa Dola za Kimarekani 55,000 (sawa na Sh. Milioni 81) kutokana na kuilipa fidia Gefle ambayo bado ina mkataba na kiungo huyo.
Boban alisaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo ya Sweden, ambayo nayo ilimnunua kwa thamani ya Dola za Kimarekani 50,000 (sawa na Sh. Milioni 74) kwa klabu yake nchini ya ‘Wekundu wa Msimbazi’, Simba.
Kiungo huyo alianza kutaka kuvunja mkataba na klabu yake hiyo tangu mwezi Aprili mwaka huu na katika jitihada za kumbakisha Ulaya, kocha mkuu wa Gefle alimtafutia timu nyingine, lakini Boban alieleza kuwa mazingira ya huko yanamuia vigumu kuendelea kucheza soka na kuwaeleza kuwa anataka kurejea Simba.
Klabu za Simba na Yanga, zinadaiwa kuwa hivi sasa ziko njia panda na zimesitisha nia ya kutaka kumsajili Boban kutokana na kuogopa ada ya uhamisho, ambayo inatakiwa kuambatana na fidia kwa klabu yake ya sasa ya Gefle IF.
Jamaa wa BBC wanasema jamaa kiwango hakuna sio matatizo ya kodi ,aache kudanganja watu.
ReplyDeleteIngekuwa mara yake ya kwanza kuvunja mkataba ningeshangaa. Karibu kitaani
ReplyDelete