Sunday, July 11, 2010

Hivi serikali maana yake ni CCM? Kweli?




Najaribu kuelewa mambo mawili matatu juu ya nchi yangu ya Tanzania. Yaani siamini kwamba nchi nzima inatega sikio kusikia ni nini kinaendelea katika mkutano mkuu wa CCM. Naweza kulaamu TBC kwa upande mmoja lakini sitakuwa fair. Ila pale itakapotokea ya kwamba hawatarusha mikatano mikuu ya vyama vingine then nitawaambia wakanyonye***
Naelewa kwamba siko peke yangu ambaye sielewi swala zima la u CCM lakini imekuwa ngumu kukutana na mtu mwingine tunayekubaliana sawasawa na kwa uwazi kuhusu ujinga huu. Nimekutana na watanzania mbalimbali ambao tumekubaliana moja kwa moja kuhusu ujinga unaondelea Bongo lakini kwa sababu moja au njingine hawapo tayari kuweka hadharani na kusimama kidete kuelezea umma wanachofikiri.
Moyoni ninaiota siku ambayo CCM hawatakuwa madarakani tena. Naota kuona mali walizojipatia kwa mgongo wa umma zikichukuliwa na serikali kwa sababu sielewi sababu yoyote iliyowafanya wakaachiwa umiliki wa vitega uchumi vyote walivyokuwa navyo wakati nchi ilipokuwa ni chama kimoja. Lazima tuelewe ya kwamba wakati wa chama kimoja serikali na chama ilikuwa ni kitu kimoja kwa hiyo mali za CCM ni mali ya serikali.
Mimi naamini kabisa ni rushwa inayofanya watanzania wote kuangalia matokeo ya mkutano mkuu wa CCM. Wagombea wa chama hiki siku zote humwaga fedha nyingi kwenye kampeni. Binafsi nafahamu watu waliojenga nyuma wakati wa kipindi cha uchaguzi. Watu wanataka kujua ni wapi kwa kupata kula.
Binafsi naona aibu ya kuwa watu wanauza kura zao kwa sababu ya njaa. Nawaonea huruma vyama vya upinzani kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kushindana. Na ninaamini baadhi ya vyama vya upinzni si vya kweli bali ni vibaraka wenye kazi ya kudhoofisha upinzani.

No comments:

Post a Comment